Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema kuwa mkutano wa Tehran uliopewa jina la 'Kuiunga Mkono Palestina, Dhihirisho la Mapambano, na Gaza Mhanga wa Jinai" ni hatua muhimu katika njia ya kutatua mgogoro wa Palestina na ni ishara ya kuwepo Palestina katika nyoyo za Waislamu.
Dakta Ramadhan Shallah amesisitiza kwamba mbali na kutayarisha mashtaka dhidi ya watenda jinai za Kizayuni wa Israe, lengo la mkutano wa Tehran ni kujenga hali ya kujiamini na kuondoa hitilafu kati ya makundi ya Palestina.
Dakta Shallah amesema kuwa chanzo cha hitilafu hizo ni kutokuwepo mtazamo mmoja kati ya vyama na makundi tofauti na kwamba suala hilo linampa adui Mzayuni visingizio mbalimbali.
Kiongozi wa harakati ya Jihad Islami ameyataka makundi yote ya mapambano ya Palestina kushikamana na kushirikiana katika kuwasaidia wananchi.
Amesema kuwa kwa sasa Ukanda wa Gaza umekuwa mithili ya jela kubwa zaidi kuliko zote duniani yenye idadi ya wafungwa milioni moja na nusu. Dakta Ramadhan Shallah amezitaka nchi za Kiarabu kutekeleza majukumu yao ya Kiislamu na kibinadamu na akatahadharisha kwamba Israel haiilengi Palestina pekee bali utawala huo wa Kizayuni unakusudia kuvuruga amani na utulivu wa nchi zote za Mashariki ya Kati.
Katibu Mkuu wa Jihad Islami ameashiria ahadi nyingi zilizotolewa kwa ajili ya misaada ya kuijenga upya Gaza na akasema, kutoa ahadi pekee hakutoshi na misaada hiyo haipaswi kukabidhiwa kwa kundi makhsusisi kwa sababu suala hilo litakuwa na madhara kwa wananchi wa kawaida. 373159