Hata kama Mustafa Ismail angali anatumia mbinu za usomaji Qur'ani zilizotumiwa na wasomaji waliomtangulia kama vile Abdulfatah As-Sha'shai, Ibrahim as-Sha'shai na Muhammad Rafa't lakini mwenyewe amegundua mbinu ya usomaji ambayo inaondoa makosa na kasoro za mbinu za wasomaji hao wa zamani.
Akizungumza na Shirika la Habari za Qur'ani Iqna, Haidar al-Kasmai Mkuu wa Jopo la Wasimamizi wa Wasomaji na Wahifadhi wa Qur'ani katika Mkoa wa Qum amesema kuwa Mustafa Ismail ni msanii aliyekuwa na kipawa kikubwa katika uwanja ya sauti na lahani, jambo ambalo limemfanya daima kuwa katika mstari wa mbele wa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani duniani.
Mtaalamu huyo wa masuala ya Qur'ani ameendelea kusema kuwa wasomaji wengi Waarabu wa Qur'ani Tukufu na hasa wa Misri, huzingatia sana maana ya kitabu hicho kitakatifu na kwamba lahani zao huenda sambamba na maana ya aya za Qur'ani. Amesema, usomaji wa Qur'ani wa Muhammad Swadiq Manshawi, Mustafa Ismail na Abdul Basit unakwenda sambamba na maana ya aya na visa vya Qur'ani Tukufu.
Mkufunzi huyo wa Qur'an amesema kuwa Marehemu Mustafa Ismail alianza usomaji wake katika radio ya Qur'ani ya Misri na kisha usomaji wake ukasambazwa katika vyombo vingine vya habari na hivyo kuleta uvumbuzi mpya katika usomaji wa Qur'ani. Amesema kuwa msomaji huyo ndiye mashuhuri zaidi baada ya Abdul Basit. 373143