IQNA

Mgawanyiko wa Shia na Sunni utaleta udhaifu miongoni mwa Waislamu

17:42 - March 07, 2009
Habari ID: 1752909
Hakuna mtu yoyote anayeweza kudhurika kutokana na umoja bali kinyume chake ni kuwa mtengano na hitilafu huwadhoofisha Waislamu, jambo ambalo huleta madhara makubwa kwa umma mzima wa Kiislamu.
Akizungumza mwishoni mwa kikao cha nne cha kimataifa cha mjini Tehran cha kuwaunga mkono Wapalestina, Ali Akbar Wilayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kisiasa ameashiria kuvunjiwa heshima matukufu ya Washia nchini Saudi Arabia na kusema kuwa licha ya kuwa hajui kwa undani kile kilichotokea hivi karibuni nchini humo dhidi ya Mashia, lakini ni wazi kuwa jambo lolote lile linalovuruga umoja wa Shia na Sunni linapasa kukemewa vikali.
Amesisitiza kwamba Waislamu wote katika kila pembe ya dunia wanapasa kujiepusha na fitina na masuala yanayozusha mgawanyiko miongoni mwao.
Inakumbushwa hapa kuwa kikao cha kimataifa cha kuwaunga mkono Wapalestina kilifanyika hapa mjini Tehran hivi karibuni chini ya anwani ya 'Palestina Dhihirisho la Mapambano, Gaza, Mhanga wa Jinai.'373607
captcha