IQNA

Ahmadinejad: Nchi zote za Kiislamu zinapaswa kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina

13:15 - March 08, 2009
Habari ID: 1753181
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa nchi zote za Kiislamu zinapaswa kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina kwa uwezo wao wote.
Rais Mahmoud Ahmadinejad aliyasema hayo katika mazungumzo yake na Maspika wa Mali na Gambia waliokuwa safarini mjini Tehran na kuongeza kuwa utawala wa Kizayuni umo katika hali ya kuporomoka na mapambano ya ukombozi wa taifa la Palestina yanakaribia ushindi.
Amesisitiza tena juu ya wajibu wa mataifa na nchi za Kiislamu kuwatetea na kuwasaidia wananchi wa Palestina kwa hali na mali. Amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa kipaumbele kwa suala la kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika na akaongeza kuwa Tehran iko tayari kutoa uzoefu wake katika nyanja mbalimbali kwa mataifa ya Afrika.
Maspika wa Mabunge ya Mali na Gambia pia wamesisitiza juu ya umuhimu wa kuwaunga mkono wananchi wanaokandamizwa wa Palestina na wakasema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfano wa kuigwa katika medani hiyo.
Waspika hao wameipongeza Iran kwa misimamo yake kuhusu nchi za Kiafrika na wakasema, Mali na Gambia zinataka kustawisha zaidi uhusiano na Tehran. 374019
captcha