IQNA

Ayatullah Khamenei:

Jukumu muhimu la wafuasi wa Mtume wa Uislamu (saw) ni kufanya juhudi za kuimarisha umoja wa Kiislamu

16:35 - March 16, 2009
Habari ID: 1756592
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa jukumu muhimu la wafuasi wa Mtume wa Uislamu (saw) ni kufanya juhudi za kujenga umoja kati ya Waislamu na kukabiliana na sababu zinazozusha mifarakano kati yao.
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo katika mazungumzo yake na wasomi na wanafikra zaidi ya 150 kutoka nj ya nchi walioshiriki kwenye Mkutano wa Kimataifa ya Umoja wa Kiislamu mjini Tehran. Amesisitiza kuwa, kuzaliwa Mtume Mtukufu wa Uislamu Muhammad (saw) lilikuwa tukio kubwa na la thamani kwa ajili ya mwanadamu.
Kiongozi Muadhamu alisema katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Iran, mabalozi wa nchi za Kiislamu na wananchi wa matabaka mbalimbali kuwa mojawapo ya majukumu makubwa ya yanayopaswa kuzingatiwa na Waislamu kuhusiana na neema ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw) ni kufanya jitihada za kivitendo ili kupatikana umoja miongoni mwa Waislamu.
Ameendelea kusema kuwa, jukumu jingine la Waislamu, bila ya kujali madhehebu zao za Shia na Suni, ni kutetea itikadi zao kwa mantiki na kutobadili vikao vya mijadala ya kielimu na kuwa vya matusi na dharau dhidi ya itikadi na imani za upande wa pili.
Akiashiria njama za maadu za kuwatenganisha Waislamu, Ayatullahil Udhma Khamenei amesisitiza kwamba Waislamu wanapasa kuwa na mipango madhubuti ya kukabiliana na njama hizo ili wasije wakakumbwa na madhara yazo.
Huku akiashiria ushindi wa Wapiganaji wa Kiislamu katika mapigano ya siku 33 huko Labanon na ya siku 22 katika Ukanda wa Gaza, Ayatullah Khamenei amesema kuwa suala la Palestina ni suala la umma mzima wa Kiislamu na kwamba halina uhusiano na Waarabu wala Waajemi. Amesema, iwapo suala hilo litabadilishwa na kuwa la kikabila, basi hicho kitakuwa ni chanzo kikubwa cha mfarakano kati ya Waislamu. 378036
captcha