Shirika la habari la Ma'an limeripoti kuwa maafisa wa kamati hiyo wameanzisha harakati kubwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa ajili ya kutoa pigo dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kupitia njia ya kususia bidhaa za utawala huo.
Maafisa wa kamati hiyo pia wamekutana na viongozi wa miji mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi na kuzungumzia suala la kuanzisha mafunzo ya jinsi ya kuzidisha harakati za kususia bidhaa za Israel na kuanzisha mapambano ya kiuchumi dhidi ya utawala huo haramu.
Viongozi wa Kamati ya Palestina inayoshughulikia suala la kusisiwa bidhaa za Israel wamekutana pia na viongozi wa jumuiya ya watengeneza mada na madaktari wa Ukingo wa Magharibi kupanga mikakati ya kususiwa zaidi bidhaa za utawala huo. 378068