Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, Kamishna wa zamani wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Mery Robinson, Richard Goldstone ambaye ni Mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, Antonio Kassesse alikuwa Mkuu wa kwanza wa Mahakama ya Kimataifa ya Kuchunguza Jinai za kivita katika Yugoslavia ya zamani ambao ni miongoni mwa wanachama wa kundi hilo, wameelezea kushangazwa mno na maafa jinai kubwa zilizofnywa na Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza na wakataka kufanyike uchunguzi mkubwa kuhusu jinai hizo.
Barua hiyo imetolewa wakati Kamati ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ikijitayarisha kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu wa umoja huo juu ya mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya taasisi za UN huko Gaza.
Barua hiyo imesisitiza kuwa uchunguzi kuhusu maafa ya Gaza haupasi kuishia kwenye taasisi za Umoja wa Mataifa.
Watu waliotia saini barua hiyo ambao waliwahi kuchunguza jinai za kivita na dhidi ya binadamu katika nchi za Ugoslavia, Afrika Kusini, Sierra Leon Timor ya Mashariki, Lebanon na Peru, wamesema kuwa wameshtushwa mno na jinai zilizofanywa na Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza.
Vilevile wamewataka viongozi wa nchi mbalimbali duniani kuvunja kimya chao na kulaani waziwazi jinai hizo ambazo zinahesabiwa na sheria zote kuwa ni mauaji dhidi ya raia wakati wa vita. 378599