Taasisi ya Matakatifu Yohana imeashiria historia mbaya ya Rasmussen na uhasama wake dhidi ya dini ya Kiislamu hususan msimamo wake wa kutetea vibonzo vilivyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) nchini Denmark na kulaani kimya cha duru za kimataifa kuhusu uteuzi wa mwanasiasa huyo kuwa mkuu wa shirika la NATO.
Taarifa ya Taasisi ya Mtakatifu Yohana imesema: Katika kipindi ambacho ulimwengu wa Kiarabu ulikuwa ukisubiri kuona marekebisho ya kimsingi katika siasa za nchi za Magharibi hususan baada ya ushindi wa chama cha Democrats huko Marekani, kuchaguliwa kwa Waziri Mkuu mbaguzi na mwenye misimamo ya kuchupa mipaka wa Denmark kuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO kutachochea hisia za mamilioni ya Waislamu kote duniani.
Taarifa ya Jumuiya ya Yohana imesisitiza kuwa kitendo hicho kitachochea mwenendo wa misimamo mikali na kukwamisha juhudi za kuimarisha amani na utulifu duniani. Imesema kuwa kuchaguliwa Rasmussen kuwa Katibu Mkuu wa NATO kuna maana ya kuunga mkono siasa za kibaguzi.
Taarifa hiyo pia imewataka viongozi wa nchi za Kiarabu kukata uhusiano na ushirikiano wao na shirika la NATO linalowaunga mkono maadui wa Uislamu. 384901