IQNA

Paris, mwenyeji wa kongamano la Vijana wa Kiislamu kwa Ajili ya Kukabiliana na Matatizo ya Kijamii

11:47 - April 12, 2009
Habari ID: 1763545
Mkutano wa Vijana wa Kiislamu kwa Ajili ya Kutafuta Suluhisho la Matatizo ya Kijamii unaanza leo katika mji wa Mantes-la-Jolie ulioko kandokando mwa mji mkuu wa Ufaransa Paris.
Mkutano huo umetayarishwa na Kituo cha Utamaduni na Elimu cha Waturuki wanaoishi nchini Ufaransa.
Washiriki katika kutano huo wanajadili na kuchunguza masuala yanayohusiana na jamii ya sasa ya Ulaya na nafasi ya vijana wa Kiislamu barani humo.
Mkutano huo utachunguza mahusiano ya wanawake na wanaume barani Ulaya, vileo, dawa za kulevya na mchango wa vijana wa Kiislamu na dini tukufu ya Kiislamu katika kukabiliana na changamoto hizo.
Mji wa Mantes-la-Jolie uko umbali wa kilomita 53 kutoka Paris. 386074


captcha