IQNA

Kuwasaidia wapiganaji jihadi wa Palestina ni wajibu wa kidini

15:01 - April 21, 2009
Habari ID: 1768035
Sheikh Sharif Tutyu ambaye ni miongoni mwa viongozi wa harakati ya Amal al Islami ya Lebanon amesema kuwa suala la kuwasaidia wapiganaji jihadi wa Palestina ni wajibu wa kidini kwa Waislamu wote.
Sheikh Tutyu amesema kuwa ni wajibu kwa Waislamu wote na wapigania uhuru wa Kiarabu kufanya jitihada za kukomboa msikiti wa al Aqsa, Quds tukufu na ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na pia kuwasaidia wapigania uhuru wa taifa hilo.
Amesema kuwa kuwasaidia wapiganaji jihadi wa Palestina hakuwezi kutambuliwa kuwa ni aibu au kukiuka usalama wa nchi yoyote, bali ni fahari kubwa na upinzani wa dhulma na mwenendo wa kusalimu amri mbele ya madhalimu.
Kiongozi huyo wa ngazi za juu katika harakati ya Amal al Islami ya Jordan amesisitiza kuwa mapambano yanayofanyika hivi sasa katika Mashariki ya Kati hususan huko Palestina ni mapambano baina ya haki na batili, kati ya dhalimu na mdhulumiwa na baina ya wavamizi na watu wanaotetea haki na ardhi zao. 391418

captcha