IQNA

Uungaji mkono wa jamii ya kimataifa kwa utawala haramu wa Israel kusiwafanye Waislamu kutofuatilia kisheria jinai za utawala huo

13:57 - April 23, 2009
Habari ID: 1768745
Ushawishi na satuwa ya madola makubwa ya Magharibi katika jumuiya na mashirika ya kimtaifa, madola ambayo yanaunga mkono kwa dhati utawala haramu wa Israel, imeufanya utawala huo kutofikishwa mbele ya vyombo vya sheria wala kufuatiliwa kisheria katika ngazi za kimataifa kutokana na jinai unazotenda katika ardhi za Wapalestina unazokalia kwa mabavu.
Akizungumzia suala hilo, Zaki Azmi, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Malaysia amesema kuwa hadi sasa kuna mashtaka 156 ambayo yamekwishawasilishwa na wakazi wa Gaza, wahanga wa mauaji ya umati kutoka kwa utawala haramu wa Israel lakini akaongeza kuwa mashtaka hayo yanatakiwa kuambatanishwa na nyaraka pamoja na ushahidi wa kutosha ili yawasilishwe katika mahakama zenye itibari za kimataifa. Azmi amesikitishwa mno na ukweli kwamba pamoja na kuwa utawala huo ulitekeleza mauaji ya umati na jinai kubwa dhidi ya watu wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza na hasa watoto na wanawake katika hujuma yake ya kinyama ya siku 22, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kisheria kwa ajili ya kuuhukumu kimataifa utawala huo kutokana na uungaji mkono mkubwa unaupata kutoka kwa madola ya kibeberu na yenye nguvu kubwa ya Magharibi. Amesema ni kutokana na suala hilo ndipo utawala huo ukaendeleza hujuma yake hiyo dhidi ya wakazi wa Gaza licha ya kuwepo maandamano makubwa yaliyofanywa katika pambe zote za dunia dhidi ya hujuma hiyo ya Wazayuni. Amesema, uungaji mkono huo wa madola ya Magharibi umeupelekea utawala huo udumishe jinai zake dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kwa kwa kuendelea kutekeleza mzingiro wa kidhulma dhidi yao, mzingiro ambao unawanyima huduma za kimsingi kabisa zikiwemo za chakula na madawa, na hata kuzuia wagonjwa kufikishwa mahospitalini kwa ajili ya kupata matibabu ya dharura. Azmi amesisitiza kwamba, iwapo watawala katili wa Israel hawatafikishwa katika mahakama za kimataifa kujibu mashtaka ya mauaji dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, ni wazi kuwa watazidi kuwakandamiza Wapestina madhlumu na pia kuendelea kuhatarisha usalama wa ulimwengu. Amesema nchi za Kiislamu zinapasa kuwa shujaa na kubuni njia za kukabiliana na uchokozi pamoja na na jinai za utawala huo. 392472
captcha