Akizungumza katika mkutano wake na familia za mashahidi na wenye kujitolea muhanga mkoani Tehran 25 Aprili, Rais Ahmadinejad amesema madola yanayotumia mabavu yanapswa kujishughulisha tu na masuala yanayowahusu. Amesema rais wa zamani wa Marekani, Bush, aliliwekea taifa la Iran masharti na natija yake iliwadhihirikia watu wote. Ameongeza kuwa Rais Barack Obama aliyechukua nafasi ya Bush sasa anasema kuwa hatua zozote zinaweza kuchukuliwa dhidi ya Iran. Rais wa Iran amesema iwapo kweli madola yanayotumia mabavu yanataka kuleta mabadiliko ya kweli, taifa la Iran litawasaidia, lakini iwapo hayajapata funzo kuhusu yaliyopita, basi yanapaswa kujifunza namna ya kuamiliana na mataifa.
Rais Ahmadinejad amesisitiza kuwa taifa la Iran litaendelea kusimama imara katika malengo yake matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu. Amesema kuwa madola yanayotumia mabavu yanapaswa kufahamu kuwa baada ya kupita miaka 30, familia za mashahidi na wanaojitolea zinasimama imara zaidi katika kutetea na kuhami mapinduzi.
394617