IQNA

Utegemezi wa kisiasa wa Baraza la Usalama unazuia kufuatiliwa jinai za Israel

10:29 - April 27, 2009
Habari ID: 1770393
Utegemezi wa kisiasa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa baadhi ya nchi wanachama wake zenye haki ya kura ya veto na matumizi mabaya ya kura hiyo vinazuia kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya jinai zilizofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika ardhi za Palestina.
Hayo yamesemwa na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sheria cha Lebanon Wasim Mansuri ambaye ameongeza kuwa, ni vigumu mno kuweza kufuatilia jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya Baraza la Usalama kwa kuzingatia kwamba baraza hilo la Umoja wa Mataifa ni taasisi ya kisiasa inayodhibitiwa na nchi wanachama wenye haki ya kutumia kura ya veto. Mwanasheria hiyo wa Lebanon amesema kuwa nchi hizo zinapiga kura ya veto dhidi ya muswada wowote unaoipinga Israel na kwa msingi huo kuna udharura wa kutafutwa njia nyingine ya kushughulikia jinai za utawala huo.
Wasim Mansuri amesema kuwa kuna haja ya kubuniwa njia na mikakati mipya ya kufuatilia jinai za utawala ghasibu wa Israel katika medani ya kimataifa.
Mwanasheria huyo amepongeza hatua ya Iran ya kuzitaka mahakama za kieneo na polisi ya kimataifa kufuatilia jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina na akasema kuwa iwapo hatua kama hizo zitachukuliwa katika nchi mbalimbali zitakuwa na taathira kubwa katika kufanikisha jambo hilo. 394021

captcha