IQNA

Katibu Mkuu wa OIC:

Siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, fursa ya kudhihirisha utambulisho wa Kiislamu

8:01 - May 04, 2009
Habari ID: 1773454
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kuwa siku ya kimataifa ya uhuru wa habari ni fursa nzuri ya kudhihirisha utambulisho wa Kiislamu, kustawisha mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali na kusaidia juhudi za kurejesha amani ya kimataifa.
Ekmeleddin Ihsanoglu amesema katika ujumbe wake uliotolewa kwa mnasaba wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa habari inayosadifiana na tarehe 3 Mei kila mwaka kwamba siku hiyo ni fursa nzuri ya kuadhimisha misingi ya uhuru wa bahari, kutathmini uhuru huo kote duniani, kuunga mkono uhuru wa vyombo vya habari na kuwaenzi wafanyakazi wake ambao wana majukumu mazito na nyeti mno.
Katibu Mkuu wa OIC amesema kuwa jumuiya hiyo itaendelea kuheshimu misingi ya uhuru wa kusema na uhuru wa habari kama sehemu ya haki za kimsingi za mwanadamu. Amesema kuwa lengo kuu la kuenziwa siku hiyo na OIC ni kuimarisha mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali, kujenga maelewano na kuondoa mivutano na ufahamu uziokuwa sahihi.
Ihsanoglu ameongeza kuwa jumuiya ya OIC inapongeza vyombo vya habari vinavyoheshimu misingi na sheria za mazungumzo na maelewano na vinavyojiepusha na hatua yoyote ya kuharibu na kuvunjia heshima matukufu ya kidini.
Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vinapaswa kujiepusha na habari zinazozusha hitilafu na kuhatarisha haki za awali za wafuasi wa dini tofauti. 398618
captcha