IQNA

Tanzania mwenyeji wa kongamano la 'Nafasi ya Imam Khomeini (SA) katika kuhuisha utambulisho wa Kiislamu'

11:56 - May 21, 2009
Habari ID: 1781120
Kongamano la 'Nafasi ya Imam Khomeini (SA) katika kuhuisha utambulisho wa Kiislamu' litafanyika Dar-es-Salaam mji mkuu wa Tanzania kwa munasaba wa mwaka wa 20 wa kumbukumbu ya kuaga dunia Imam Khomeini (SA).
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limeandaliwa na Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar-es-Salaam.
Kati ya programu nyinginezo zilizoandaliwa kwa munasaba huo ni hafla maalumu katika Makao ya Balozi wa Iran mjini Dar-es-Salaam na kusambazwa vitabu kuhusu maisha ya kisiasa ya Imam Khomeini (SA) kwa lugha ya Kiswahili huko Tanzania na Kenya na nchi zote zinazozungmza lugha ya Kiswahili katika eneo.
Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar-es-Salaam imeongeza kuwa, filamu ya maisha ya Imam Khomeini (SA) itarushwa hewani katika vituo mbali mbali vya televisheni Tanzania kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza mbali na kuchapishwa makala katika magazeti ya nchi hiyo. 408406
captcha