Makundi hayo yameshambulia misikiti kadhaa ya Waislamu wa Kishia na kuua Waislamu kadhaa wasiokuwa na hatia. Maandamano hayo yameitishwa na Jumuiya ya Maulamaa wa Kishia wa Pakistan kwa shabaha ya kulaani mauaji na jinai zinazoendelea kufanywa na makundi ya Kiwahabi.
Sayyid Sajid Ali Naqawi ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu wa Pakistan amewataka Waislamu wa Kishia kushiriki kwenye maandamano kama hayo ya kulaani jinai na ukatili wa makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka ya Kiwahabi.
Vyama na jumuiya mbalimbali za Waislamu wa Kishia wa Saudi Arabia zimetoa taarifa mbalimbali zikilaami mauaji yanayofanyw ana makundi ya Kiwahabi dhidia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia huko Pakistan. 429538