IQNA

Mkutano wa Baraza la Waasisi wa Shirikisho la Ulimwengu wa Kiislamu waanza Makka

12:49 - August 04, 2010
Habari ID: 1967057
Mkutano wa Baraza la Waasisi wa Shirikisho la Ulimwengu wa Kiislamu (Muslim World League) ulianza jana mjini Makka Saudi Arabia ukihudhuriwa na Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri.
Mkutano huo unaongozwa na Mufti wa Saudia Sheikh Abdul Aziz bin Abdullah Al al Sheikh ambaye pia ni kiongozi wa Baraza la Waasisi wa Shirikisho la Ulimwengu wa Uislamu.
Mkutano huo unahudhuriwa na maulama na wanafikra wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali duniani.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ulimwengu wa Kiislamu Abdullah Abdul Muhsin al Turki amesema kuhusu suala hilo kwamba kikao cha Baraza la Kimataifa la Misikiti kitaanza pia kazi zake leo katika mji mtakatifu wa Makka. Al Turki amesisitiza kuwa vikao vya mikutano hiyo vinahudhuriwa na wasomi na wanafikra wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali na kwamba hiyo itakuwa fursa ya kujadili matatizo na changamoto zinazowakabili Waislamu katika maeneo mbalimbali na kutafuta njia za ufumbuzi wake. 625814
captcha