IQNA

Ubalozi wa Iran Tanzania kuwaandalia futari mabalozi wa nchi za Kiislamu

19:26 - September 01, 2010
Habari ID: 1985829
Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania umewaalika shakhsia wa kisiasa na mabalozi wanaowakilisha nchi Kiislamu nchini Tanzania katika dhifa ya futari.
Bw. Mostafa Ranjbar Shirazi Mkuu Idara ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa dhifa hiyo ya futari itafanyika wiki hii mjini Dar-es-Salaam kwa lengo la kutangaza harakati za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni.
Ameongeza kuwa Ijumaa iliyopita Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar-es-Salaam uliandaa dhifa ya futari iliyohuduriwa na shakhsia 180 wa kiutamaduni na kidini nchini Tanzania.
646097
captcha