Katika kikao chao kilichofanyika siku ya Ijumaa huko mjini New York Marekani, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, walibainisha wasiwasi na masikitiko yao makubwa kuhusiana na kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Imarati WAM, mawaziri hao walitoa taarifa mwishoni mwa kikao chao wakiitaka jamii ya kimataifa kuzuia vitendo vya dharau dhidi ya matukufu ya dini ya Kiislamu na chuki dhidi ya Waislamu walio wachache katika jamii za Magharibi.
Taarifa hiyo pia imeishukuru Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC kwa kufanya juhudi za kupitishwa azimio la kuzuia dharau dhidi ya matukufu ya kidini katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Pia imezishishukuru taasisi za kidini ambazo zimelaani na kukemea kitendo cha makundi yaliyo na misimamo ya kupindukia mipaka nchini Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu.
Katika taarifa hiyo, Mawaziri wa Mambo ya Nje wanachama wa OIC wamelaani kuongezeka mielekeo ya chuki dhidi ya Uislamu katika jamii za Magharibi na kusifu hatua ya kuasisiwa jumuiya ya kuimarisha shughui za wanawake wa Kiislamu katika jamii mjini Cairo. 662519