IQNA

Kuruhusiwa hijabu kwa mfanyakazi wa Kiislamu mjini California

11:16 - September 29, 2010
Habari ID: 2003798
Wakurugenzi wa bustani ya Disneyland katika jimbo la California wamemruhusu mfanyakazi mmoja wa Kiislamu kuendelea na kazi yake huku akiwa amevalia vazi la hijabu.
Awali mfanyakazi huyo wa kike alikuwa amezuiwa kuvaa vazi hilo kazini. Kwa mujibu wa gazetila Los Angeles Times mfanyakazi huyo ambaye ni mwenyeji wa Chicago ambaye aliajiriwa na wasimamizi wa bustani hiyo kama mratibu wa masuala ya likizo kupitia mazungumzo ya simu, alisailiwa na wasimamizi hao baada ya kuonekana kazini akiwa amevalia hijabu.
Baada ya muda fulani, wasimamizi hao walimzuia aendelee na kazi hadi wakati wa kufumwa sare yake maalumu ambayo inaambatana na sheria za Kiislamu, jambo ambalo walisema lingechukua muda wa miezi mitano yaani hadi wakati wa kumalizika kipindi alichopewa kuhudumia idara ya bustani hiyo. Lakini kufuatia uingiliaji kati wa Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Marekani, wasimamizi hao walimruhusu aendelee na kazi yake hadi wakati wa kuwa tayari vazi hilo.
Siku chache zilizopita pia mwanamke mmoja wa Kiislamu aliyekuwa akifanya kazi katika moja ya mikahawa ya Disney alifukuzwa kazi kutokana na uamuzi wake wa kuvaa hijabu kazini licha ya kukatazwa kufanya hivyo. Mfanyakazi huyo alifikisha malalamiko yake mahakamani na kwa mujibu wa baraza hilo bado malalamiko hayo yanashughulikiwa. 664825
captcha