IQNA

Onyo la shakhsia wa Kiislamu na Kikristo dhidi ya kufutwa utambulisho wa kidini wa Quds Tukufu

13:47 - October 09, 2010
Habari ID: 2009071
Wakizungumza katika mkutano wa waandishi habari huko Ramallah katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, shakhsia wa Kiislamu na Kikristo wa Palestina wameonya dhidi ya kupotoshwa na kufutwa utambulisho wa kidini wa Quds Tukufu na kusisitiza kwamba eneo hilo takatifu hivi sasa linakabiliwa na hatari kubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Kwa mujibu wa gazeti la Imarati la al-Khaleej, mkutano huo wa waandushi habari ambao umeitishwa na Baraza la Kiislamu na Kikristo la Kutetea Quds umetaka kutelezwa kwa mpango wa nchi za Kiislamu na Kiarabu wa kuwaunga mkono kifedha na kimaanawi wakazi wa Quds katika kupambana na njama za maghasibu wa Kizayuni katika mji huo. Umewataka Waislamu na Waarabu kuchukua hatua za dharura kuhusiana na jambo hilo bila kuchelewa.
Hassan Khatir, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiislamu na Kikristo la Quds ametahadharisha dhidi ya hatua za Wazayuni za kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi na kufutwa athari za matukufu ya Kiislamu na Kiarabu huko Quds na kusisitiza kwamba jambo hilo linatekelezwa kwa lego la kufuta utambulisho halisi wa kidini wa mji huo mtakatifu.
Amesema katika kikao chao cha hivi karibuni katika mji wa Sirte nchini Libya, viongozi wa Kiarabu walichukua uamuzi wa kutetea kwa kila njia quds Tukufu, jambo ambalo amelitaja kuwa ni la kutia moyo na hatua sahihi kuhusu suala hilo.
Viongozi wa Kiarabu pia katika kikao hicho walichukua uamuzi wa kuandaa kikao cha kimataifa huko Qatar kwa lengo la kuimarisha mwamko wa kutetea Quds miongoni mwa nchi za Kiarabu na Kiislamu. 670544
captcha