Waislamu hao wamesema kuwa kuwepo kwa mbuge huyo aliyehujumu Uislamu katika jamii ni hatari kubwa.
Shirika la bahari la UFaransa (AFP) limeripoti kuwa watu waliowasilisha mashtaka dhidi ya Wilders walitangaza jana katika Mahakama ya The Hague kwamba kuwepo mbunge huyo katika jamii ya Uholanzi kutazusha hitilafu kati ya raia na jambo hilo ni hatari kubwa.
Nawal Ubaida ambaye ni miongoni mwa waliowasilisha mashtaka dhidi ya mbunge huyo mbaguzi amesema kuwa Geert Wilders ni mnadharia wa fikra za kibaguzi ambazo zimezusha mifarakano na machafuko katika jamii. Amesema kuwa mhakama unapaswa kuwalinda Waislamu kutokana na mitazamo ya kibaguzi ya mbunge huyo.
Muhammad Rubai ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wa Uholanzi ameiambia Makahama ya The Hague kwamba kila siku Waislamu wa nchi hiyo wanakabiliwa na hujuma za kibaguzi na watoto wao hawana matumaini ya mustakbali mwema kutokana na anga iliyojaa hujuma na matamshi ya kibaguzi ya mbunge Wilders dhidi ya Waislamu.
Mbunge huyo wa Uholanzi aliukasirisha ulimwengu mzima wa Kiislamu baada ya kutengeneza filamu ya Fitna inayokivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani na kudhalilisha matukufu mengine ya dini hiyo. 678187