Sayyid Husseini amesema kuwa katika hali ya sasa kuna wimbi kubwa la propaganda chafu katika nchini za Magharibi dhidi ya Uislamu na nchi hizo zinatumia nyenzo za kipropaganda, televisheni na redio kwa ajili ya kuhujumu thamani na matukufu ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa mamia ya filamu zimetengenezwa katika Hollywood kwa shabaha ya kuchafua sura ya Uislamu na Waislamu na mfano wa karibuni wa propaganda hizo chafu ni katuni zinazomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani.
Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema kuwa Wamagharibi wameelekeza mishare yao dhidi ya Uislamu na ni wajibu wa vyombo vya habari vya nchi za Kiislamu kufichua hujuma na njama hizo.
Amesema kuwa inasikitishia kuona kwamba Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC haitekekelezi vyema wajibu wake wa kutetea Uislamu na Waislamu. Amesisitiza kuwa Wamagharibi wanadai kuwa Waislamu ni wapenda vita na machafuko ilhali nchi hizo hizo za Magharibi zimeshambulia mataifa ya Kiislamu na kuzikalia kwa mabavu nchi za Iraq na Afghanistan kwa kisingizio cha matukio ya Septemba 11.
Akijibu swali kwamba ni hatua gani zilizochukuliwa na Iran kupambana na hujuma hizo, Sayyid Hussein amesema Tehran imechukua hatua ya kuanzisha kanali mbili za televisheni za kimataifa kwa lugha za Kiarabu na Kiingereza na kuitisha makongamano na mikutano ya mara kwa mara ya kimataifa ya kutangaza sura halisi ya Uislamu na Iran. 684087