IQNA

Masomo katika nchi za Kiarabu, kisingizio cha watawala wa Uzbekistan kuwafuta kazi wafanyakazi wa Kiislamu

11:44 - April 09, 2011
Habari ID: 2102526
Wimbi la mwamko linaloendelea kushuhudiwa katika nchi za Kiarabu limewatia wasiwasi mkubwa viongozi wa Uzbekistan na kuwapelekea kuwafuta kazi wafanyakazi wa taasisi za kidini, misikiti na shule za kidini waliosoma katika nchi za Kiarabu.
Wasiwasi huo unatokana na dhana yao kwamba huenda wafanyakazi hao wakawashawishi wananchi wa Uzbekistan kufanya maandamano kama yale yanayoendelea katika nchi za Kiarabu dhidi ya serikali ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa tovuti ya www.ca-news.org, wafanyakazi wa taasisi zilizotajwa wamekuwa wakifutwa kazi na serikali katika siku za hivi karibuni kutokana na hofu hiyo ya watawala wa Uzbekistan. Wengi wa wafanyakazi waliofukuzwa kazi walisomea masomo ya kidini katika nchi za Misri, Saudi Arabia na Libya. 770731
captcha