Kikao hicho ambacho kitahudhuriwa na wanazuoni na wasomi wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za dunia kitajadili hali ya hivi sasa ya Waislamu na matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu pamoja na njia za kuyatatua. Akizungumzia suala hilo Abdallah bin Abdul Muhsin at-Turki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu ameashiria umuhimu wa kufanyika kikao kama hicho na kuongeza kuwa jumuiya hiyo imekuwa ikifuatilia kwa karibu matatizo ya nchi za Kiislamu na kujaribu kunufaika na fikra za wasomi na wanafikra wa Kiislamu katika kuyatatua. 777614