Kwa mujibu wa tovuti ya Lexpress, habari hiyo imefichuliwa na Halmashauri ya Uhusiano wa Marekani na Uislamu CAIR na kwamba uchunguzi kuhusu jambo hilo ungali unaendelea. Halmashauri hiyo inasema kuwa, baada ya kukabiliwa na mashinikizo ya Waislamu, mkuu wa shirika la Air France nchini Ufaransa ameahidi kuchunguza tukio hilo la kusikitisha na la chuki dhidi ya Uislamu.
CAIR wakati huohuo imelitaka shirika hilo limrejeshe kazini mwanamke huyo wa Kiislamu haraka iwezekanavyo.
Hadi sasa hakuna habari kamili ambazo zimetolewa kuhusiana na shughuli hasa ya mwanamke huyo katika shirika hilo. 814166