Kituo cha habari cha Enferaad kimeripoti kuwa Sheikh Ali al Hudhaifi amefutwa kazi kutokana na hotuba yake katika Swala ya Ijumaa iliyopita mjini Madina alipowavunjia heshima Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Katika hotuba hiyo Sheikh al Hudhaifi aliwatukana Mashia kuwa ni watu walioondoka katika dini ya Kiislamu na ni makafiri.
Vilevile aliwashambulia Waislamu wa madhehebu ya Shia wa mashariki mwa Saudi Arabia wanaoandamana wakidai haki zao za kijamii na kusema kuwa wanapaswa kunyang'anywa uraia.
Matamshi hayo ya aliyekuwa Imam wa Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina yamekabiliwa na upinzani mkali wa maulamaa na wanazuoni wa Kiislamu wa Saudia Arabia akiwemo kiongozi wa Mashia wa Saudia Sheikh Hassan Saffar ambaye amesema maulamaa wa Kiwahabi wana ajenda ya kuzusha fitina na hitilafu za kimadhehebu kati ya Waislamu. 878908