IQNA

Viongozi wa Kiislamu wa Jordan wataka kufutiliwa mbali mkataba wa nchi hiyo na Israel

18:50 - October 26, 2011
Habari ID: 2212490
Viongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Jordan jana Jumanne walitoa taarifa wakitaka kufutwa mara moja mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya nchi hiyo na utawala haramu wa Israel unaojulikana kwa jina la Wadi Araba.
Kwa mujibu wa gazeti la as-Sabil linalochapishwa Jordan, kundi hilo la Kiislamu limekuwa likipinga mkataba huo tokea ulipotiwa saini mwaka 1994. Limekuwa likitaka mkataba huo ufutiliwe mbali na balozi wa utawala haramu wa Israel afukuzwe nchini humo mara moja.
Harakti hiyo ya Kiislamu imekosoa vikali kimya cha nchi za Kiarabu na Kiislamu kuhusiana na matukio ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel na pia uchokozi na dharau inayofanywa mara kwa mara na utawala huo dhidi ya matukufu ya Kiislamu kwa madhumuni ya kuzibadilisha ardhi za Palestina kuwa za Kiyahudi.
Imesema kuwa wananchi wa Palestina wataendelea kutetea Msikiti wa al-Aqsa na suala la Palestina kwa nguvu zao zote na kupinga juhudi zote za kuboresha uhusiano na utawala huo. 887452
captcha