Imewashukuru pia wananchi wote wa nchi hiyo kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huo wa kwanza wa kidemokrasia. Imesema kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huo wa bunge ambalo litabuni katiba mpya ya Tunisia, wananchi hao wamepiga hatua muhimu katika kujiainishia mustakbali wao.
Taarifa ya Hizbullah imesema kwamba ushiriki mkubwa wa Watunisia katika uchaguzi wa hivi karibuni kwa mara nyingine tena umethibitisha wazi kwamba kila taifa linalotaka kuishi kwa utukufu na heshima kamwe haliwezi kuacha mapambano ya kufikia lengo hilo na kuwa litaendelea kupigania kwa uwezo na irada yake yote mustakbali na historia yake.
Taarifa ya Hizbullah imeyataka makundi ya Kiislamu ya Tunisia kufanya kila liwezekanalo ili kutekeleza matakwa ya mashahidi na wananchi wa nchi hiyo ambao wamejitolea mhanga kwa shabaha ya kulinda kujitawala, uadilifu na utukufu wa nchi hiyo. 888140