IQNA

Wanaharakati wa Saudia wamtaka mwanamfalme wa nchi hiyo kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa

11:55 - October 30, 2011
Habari ID: 2214193
Kundi la waandishi, wasomi na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu wa Saudi Arabia wametoa taarifa wakimtaka Naif bin Abdul Aziz, mwanamfalme mpya wa nchi hiyo awaachilie huru wafungwa wote wa kisiasa wanaoteseka katika jela za nchi hiyo.
Taarifa hiyo inasema kwamba suala la wafungwa wa kisiasa wanaozuiliwa kwenye jela za utawala wa Saudia ni jambo muhimu linalowashughulisha wananchi, taasisi na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu.
Taarifa hiyo imemtaka mwanamfalme huyo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia achukue hatua za haraka ili kuhakikisha kwamba wafungwa hao wa kisiasa wanaachiliwa huru mara moja.
Mashirika ya habari ya kimataifa yalitangaza hivi karibuni kwamba utawala wa Saudia umewatia nguvuni maelfu ya wanasiasa wa nchi hiyo bila kuchukua hatua yoyote ya kuwafikisha mahakamani. 889194
captcha