IQNA

Mufti wa Misri asifiwa kwa kuwausia Wamisri kutumia barua ya Imam Ali katika katiba ya nchi hiyo

16:47 - January 16, 2012
Habari ID: 2258006
Baraza Kuu la Waislamu wa Madhehebu ya Shia nchini Misri limempongeza Mufti wa nchi hiyo kwa kuwausia Wamisri kutilia maanani na kuiga yaliyomo katika barua ya Imam Ali bin Abi Twalib kwa gavana wake wa Misri Malik al Ashtar wakati wa kutunga katiba yao mpya.
Baraza Kuu la Aalul Bait la Misri limemtumia barua Mufti Ali Guma wa nchi hiyo likisema: "Matamshi yako kwamba barua ya Imam Ali bin Abi Twalib kwa gavana wake wa Misri Malik al Ashtar inapaswa kutiliwa maanani katika uandishi wa katiba, ni ishara kwamba mheshimiwa unaitakia kheri nchi hii."
Barua hiyo ambayo imetiwa saini na wajumbe wa Baraza Kuu la Aalul Bait la Misri imesema: "Japokuwa kumefanyika mapinduzi nchini Misri lakini mabaki ya makundi ya Kiwahabi yangali yanadhibiti nchi na kundi hilo la Kiwahabi ndio Khawarij wa zama jizi na hatari kubwa kwa kwa Misri.
Ijumaa iliyopita Mufti Ali Guma wa Misri alisema katika hotuba za Swala ya Ijumaa kwamba barua ya Sayyidna Ali (as) kwa Malik al Ashtar, mtawala wa wakati huo wa Misri inastahiki kupewa umuhimu katika uandishi wa katiba ya Misri.
Imam Ali bin Abi Twalib (as) alimwandikia barua hiyo Malik Ashtar baada ya kumpa uongozi wa Misri. 935974




captcha