IQNA

Woga wa kutekelezwa fatuwa ya Imam Khomeini wamlazimishaRushdie kutupilia mbali safari ya India

16:49 - January 21, 2012
Habari ID: 2260705
Salman Rushdie, mwandishi wa kitabu cha 'Aya za Shetani' ambaye Imam Ruhullah Khomeini alitoa fatuwa akiwataka Waislamu kote duniani watekeleze hukumu ya kifo dhidi yake, ametupilia mbali nia yake ya kwenda nchini India kwa ajili ya kushiriki kwenye tamasha ya fasihi ya nchi hiyo kwa hofu ya kuuawa.
Murtadi Salman Rushdie amefuta safari hiyo kutokana na maandamano makubwa ya Waislamu wa India wanaopinga safari hiyo na kwa kuogopa uwezekano wa kutekelezwa fatuwa na Imam Khomeini na Waislamu wa India.
Murtadi Rushdie alitazamiwa kuhutubia katika siku ya ufunguzi wa Tamasha ya Fasihi Jaitapur mjini New Delhi lakini amelazimika kufuta safari ya kwenda India kushiriki katika tamasha hiyo kutokana na malalamiko ya makundi mbalimbali ya Waislamu nchini humo na kuhofia kifo.
Jana Ijumaa Waislamu wa India walikuwa wamepanga kufanya maandamano makubwa kupinga safari ya murtadi huyo lakini walifuta maandamano hayo baada ya polisi kuwahakikishia kwamba Salman Rushdie hatashiriki tena katika tamasha hiyo.
Makundi mbalimbali ya Kiislamu ya India yamewashukuru Waislamu kwa kufanikisha suala la kuzuia safari ya murtadi Rushdie nchini humo na kusema kuwa kufutwa safari yake huko India ni ushindi mkubwa.
Salman Rushdie mwenye umri wa miaka 65 alizaliwa katika mji wa Mumbai nchini India na mwaka 1988 alichapisha kitabu cha Aya za Shetani kunachomdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na matukufu mengine ya kidini, suala ambalo liliwakasirisha Waislamu kote duniani. Nchi nyingi duniani ikiwemo India zimepiga marufuku kitabu cha Aya za Shetani. Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini alitoa fatua akiwaamuru Waislamu kote duniani kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Salman Rushdie popote pale atakapokuwa. 938559
captcha