IQNA

Waziri Mkuu wa Italia awataka viongozi wa Ulaya kufanya mazungumzo na Waislamu

20:15 - May 05, 2012
Habari ID: 2318884
Waziri mkuu wa zamani wa Italia Massimo D'Alema amewataka viongozi wa nchi za Ulaya kutilia maanani zaidi suala la kufanya mazungumzo na ulimwengu wa Kiislamu.
D'Alema ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo barani Ulaya ameyasema hayo katika mkutano wa vyombo vya habari vya na kusisitiza juu ya umuhimu wa mapinduzi ya hivi karibuni katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika. Amesema kuwa matukio hayo si ya muda mfpi na ya kupita bali ni uhakika utakaoendela na kuwa na taathira nzuri kwa hali ya maeneo hayo.
D'Alema amesisitiza kuwa wanasiasa wa Ulaya wanapaswa kuwa na uhusiano mwema na viongozi wa nchi za Kiislamu na Kiarabu na amewataka watilie maanani umuhimu wa Uislamu wa kisiasa kwa Waislamu.
Waziri mkuu wa zamani wa Italia ameongeza kwamba, kuwa na uhusiani mwema na ulimwengu wa Kiislamu hakuna maana ya kutambua rasmi makundi yenye misimamo mikali.
Masimo D'Alema amesema ana matumaini kwamba serikali ya Italia itachukua hatua nzuri za kutatua ugomvi wa Palestina na utawala ghasibu wa Israel na kusaidia juhudi za kutatuliwa mgogoro wa Mashariki ya Kati. 1000241


captcha