IQNA

Lebanon yafanya juhudi za kuachiliwa raia wake waliokamatwa na magaidi wa Syria

19:10 - May 23, 2012
Habari ID: 2332784
Viongozi wa Lebanon wanafanya juhudi kubwa za kachiliwa huru wafanyaziara 11 wa Lebanon waliotekwa nyara na magenge ya magaidi wa Syria wakiwa njiani kurejea nchini kwao wakitokea nchini Iran.
Raia hao wa Lebanon walitekwa nyara katika eneo la I'zaz karibu na mji wa Halab nchini Syria. Gavana wa Mkoa wa Halab amesema kwamba wafanyaziara hao waliokuwa wanarejea Lebanon kupitia Syria kwa njia ya ardh walitekwa nyara katika mpaka wa nchi hiyo na Uturuki. Amesema watekajinyara walisimamisha mabasi mawili yaliyokuwa yamewabeba wafanyaziara hao na kuwateka nyara wanaume huku wakiwaachilia huru wanawake waliokuwa humo. Kuhusu suala hilo Adnan Mansur, Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon jana usiku aliwasiliana kwa njia ya simu na Nabil al-Arabi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kujadili udharura wa kuachiliwa huru mara moja wafanyaziara hao wa Lebanon. Waziri huyo wa Mmabo ya Nje wa Lebanon pia amewasiliana na mawaziri wenzake wa nchi za Uturuki, Syria, Kuwait na Iraq na kujadiliana nao kuhusu jambo hilo. Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon pia amekuwa akifanya mashauriano na viongozi wa makundi mbalimbali ya kisiasa ya nchi hiyo ili kuachiliwa huru raia hao wa Lebanon. Tokea kuanza machafuko huko Syria mwezi Machi mwaka uliopita, makundi ya kigaidi yanayobeba silaha yamekuwa yakijishughulisha na vitendo vya mauaji dhidi ya raia wa nchi hiyo na utekaji nyara dhidi ya raia wa nchi za kigeni wakiwemo wa Iran na Lebanon.
1014786
captcha