Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Ethiopia wamesema kuwa Yusuf Qatasho, mwandishi wa nchi hiyo ametiwa nguvuni na maafisa wa usalama kwa kuakisi habari zinazohusiana na malalamiko ya hivi karibuni ya Waslamu nchini humo.
Jumuiya ya Kutetea Waandishi wa Magazeti ya Ethiopia imesema kwamba askari usalama wa nchi hiyo walimtia mbaroni mwandishi huyo mara tu baada ya kuakisi habari inayohusiana na kukandamizwa Waislamu waliokuwa wakilalamikia serikali na askari usalama wa nchi hiyo wiki tatu zilizopita.
Mwandishi huyo ambaye amekuwa akikosoa vikali hatua ya serikali ya Ethiopia ya kuingilia masuala ya dini tofauti za nchi hiyo alitiwa nguvuni wiki tatu zilizopita na hajaonekana wala jamaa zake hawaruhisiwi kumtembelea kizuizini. Tokea atiwe mbaroni, wakili wake ameruhusiwa kuonana naye mara moja tu na tokea wakati huo hajaruhusiwa tena kuzungumza wala kuonana naye.
Mwandihi huyo wa Kiislamu anatuhumiwa na serikali kwa kuandika habari zinazodaiwa kuwa ni za kichochezi dhidi ya serikali kwa lengo la kuvuruga utulivu wa nchi hiyo.
Jumuiya iliyotajwa imelaani vikali kubanwa uhuru wa waandishi habari wa nchihiyo na kuitaka serikali imwachilie huru mara moja mwandishi huyo. 1076427