Rais Muhammad Mursi wa Misri atashiriki katika mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) mjini Tehran na kuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu wa nchi hiyo kuitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapo mwaka 1979.
Kabla ya safari yake nchini Iran ambako ataungana na viongozi wengine wa nchi za jumuiya ya NAM, Mursi atafanya safari ya siku mbili nchini Uchina.
Baada ya mkutano huo wa Tehran Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakadhidhi uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa Misri.
Safari hiyo ya Rais Muhamamd Mursi itakuwa na kwanza ya kiongozi wa ngazi za juu wa Misri mjini Tehran baada ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na baada ya kung'olewa madarakani serikali ya kidikteta ya Hosni Mubarak huko Misri. 1080744