IQNA

Viongozi Waislamu na Wakristo wapinga filamu inayomdhalilisha Mtume (saw)

19:59 - September 19, 2012
Habari ID: 2415493
Viongozi wa Kikristo na Kiislamu wa Marekani wamelaani filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na machafuko yaliyosababishwa na filamu hiyo ambayo wamesema yamechafua sura ya Waislamu duniani.
Viongozi hao wamekusanyika Los Angeles na kupinga filamu hiyo na machafuko iliyosababisha na kutoa wito wa kufanyika mazungumzo ya kupunguza mivutano na mapigano yaliyosababishwa na kuonyeshwa filamu.
Viongozi hao wamedai kuwa wapinzani wa filamu hiyo wanaotumia ghasia na machafuko hawauheshimu Uislamu wenyewe kwa sababu kusamehe ni moja ya mafunzo muhimu ya Uislamu.
Mahir Hajhuj ambaye ni mshauri wa Baraza la Masuala ya Waislamu wa Los Angeles amesema haipasi kutumia mabavu kwa ajili ya kupinga vitendo kama hivyo vya kuuvunjia heshima Uislamu.
Amesema kuwa sira ya Nabii Muhammad (saw) inatufunza kwamba wakati mtu mjinga anapokutusi muombee dua na uachane naye na usitumie suala hilo kufanya ghasia na fujo. 1102493


captcha