IQNA

Rais wa Mauritania atakiwa kuingilia kati ili Madrassah za Qur’ani zifunguliwa upya

21:38 - February 07, 2016
Habari ID: 3470120
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Nema kaskazini mashariki mwa Mauritania ametoa wito kwa rais wa nchi hiyo kuingilia kati ili madrassaha za Qur’ani zilizofungwa zifunugliwe upya.

Sheikh Muhammad al-Amin Yusuf amekosoa kuendelea kufungwa madrassha za Qur’ani nchini humo.

Amesema mamia ya wanafunzi katika shule zilizofungwa wanakosa masomo yao ya Qur’ani na hili ni jambo lilisilokubalika.

Ametoa wito kwa Rais Mohammad Ould Abdel Azizi kuingilia kati na kuzuia kulengwa taasisi za Qur’ani.

Ikumbukwe kuwa Desemba mwaka jana, kulifanyika maandamano maeneo kadhaa ya Mauritania kulaani hatua ya serikali kufunga vituo kadhaa vya Qur’ani na chekechea.

Viongozi wa kidini na wahubiri nchini humo nao pia wameonya kuhusu kuvurugwa masomo ya kidini na Qur’ani nchini humo.

Serikali ya Mauritania imeanzisha sheria mpya kuhusu usimamizi wa shule au madrassah za Qur'ani nchini humo.

Mauritania ni nchi ya eneo la Maghreb huko magharibi mwa Afrika Kaskazini na inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 4 ambao karibu wote ni Waislamu.

3473325

captcha