IQNA

Msikiti mkongwe zaidi ambao ungali unatumika Afrika Mashariki uko Zanzibar, ulijengwa na Wairani +PICHA

15:49 - December 08, 2016
Habari ID: 3470725
IQNA: Msikiti wa Kizimkazi ni kati ya misikiti mikongwe zaidi Afrika Mashariki na uko visiwani Zanzibar na ulijengwa na Wairani mwaka 500 Hijria Qamaria sawa na mwaka 1107 Miladia.

Kwa mujibu wa nyaraka za historia msikiti huo ulijengwa miaka kadhaa baada ya kuingia wahajiri kutoka Shiraz nchini Iran. Wanahistoria wanasema Msikiti wa Kizimkazi ulijengwa kufuatia amri mwanamfalme wa Kishirazi aliyekuwa miongoni mwa wahajiri waliokuwa wamewasili eneo hilo.

Msikiti wa Kizimkazi ni thibitisho kuwa katika karne ya 11 CE (AD)  Zanzibar tayari ilikuwa na Waislamu wengi.

Murtadha Ridhwanifar mjumbe wa Kituo cha Utafiti cha Shrika la Utamaduni na Utalii la Iran ambaye ametembelea Kenya na Tanzania kwa ajili ya kutayarisha orodha ya kitaalamu ya athari za kongwe za Kiirani katika nchi hizo ameutembelea Msikiti wa Kizimkazi. Katika mazungumzo na IQNA amebainisha kuhusu historia ya Msikiti wa Kizimkazi na kuutaja kuwa msikiti mkongwe zaidi ambao ungali unatumika Afrika Mashariki. Anasema uchunguzi umebaini kuwa msikiti huu ulijengwa miaka 938 iliyopita.

Ridhwanifar anaongeza kuwa, "kama ambavyo imeandikwa katika ubao ulio nje ya msikiti huo na pia kwa mujibu wa ripoti ya Neville Chittick, mwanahistoria na mtaalamu wa masuala ya kale Afrika Mashariki, iliyo katika Makavazi ya Nyaraka za Kitaifa Zanzibar, katika Msikiti wa Kizimkazi kuna jiwe lililojengwa mihrabu ambalo limeandikwa kwa nakshi za herufi za Kufi ambalo linaeleza msikiti huo mwanzo ulijengwa mwaka 500 Hijiria sawia na 1107 CE (AD) na jiwe jingine linaonyesha tarehe ya kukarabatiwa kuwa mwaka 1148 Hijria Qamaria. Msikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHA

Murtadha Ridhwanifar

Katika vigae vya Msikiti wa Kizimkazi kuna jina la Fatima Zahra SA na msikiti wote umejengwa kwa mbinu ya ujenzi wa misikiti ya zama za watawala wa Kiseljuki (Seljukid Dynasty) nchini Iran .

Ridhwanifar anasema msanifu wa majengo aliyehusika katika ujenzi wa msikiti huo alikuwa mtu mwenye jina la Kizi ambaye baada ya kukamilisha ujenzi huo aliuawa kwa amri ya Sultani. Kwa msingi huo msikiti huo ukawa mashuhuri kama Kizimkazi (yaani msikiti ambao ulijengwa kutokana na kazi ya mikono ya Kizi). Nje ya msikiti huo kuna makaburi ya kale ya Masharifu na pia kuna kaburi linalonasibishwa na Kizimkazi mwenywe.

Msikiti wa Kizimkazi ungali unatumiwa na Waislamu wa eneo hilo na ni moja kati ya turathi muhimu zaidi za kihistoria Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Msikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHA
Msikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHA
Msikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHAMsikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHAMsikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHAMsikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHAMsikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHAMsikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHAMsikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHA
Msikiti mkongwe zaidi Afrika Mashariki ulijengwa na Wairani +PICHA

3552006/

captcha