IQNA

Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran kufanyika Aprili

23:42 - December 29, 2017
Habari ID: 3471331
TEHRAN (IQNA)-Duru ya 35 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatafanyika mwezi Aprili,2018, waandalizi wamesema.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yamepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran kaunzia Aprili 19-26.

Shirika la Waqfu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaa mashindano hayo ya kila mwaka ambapo huwa na washiriki kutoka kila kona ya dunia.

Mashindano yaliyopita yalifanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA hapa mjini Tehran na inatazamiwa kuwa mashindano ya mwaka 2018 yatafanyika katika ukumbi huo huo.

Nchi ambazo zinakusudia kutuma washiriki katika mashindano hayo zinapaswa kuwasilisha majina ya washiriki kabla ya Februari nne. Halikadhalika kwa mujibu wa kanuni zilizopo, wale waslioshiriki katika mashindano ya miaka mitatu iliyopita hawataweza kushiriki katika mashindano ya 2018.

Sawa na mashindano ya mwaka 2017, Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran, pia yatakuwa na vitengo maalumu vya wanawake, wenye ulemavu wa macho na pia mashindano maalumu ya wanachuo wa vyuo vya kidini nchini Iran.

Kauli mbiu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran mwaka 2017 ilikuwa ni "Kitabu Kimoja Umma Moja" kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu ya umoja baina ya Waislamu.

3676836

captcha