IQNA

Ayatullah Araki: Waislamu waliowengi wanataka Umoja wa Kiislamu

10:32 - November 11, 2019
Habari ID: 3472210
TEHRAN (IQNA) - Waislamu waliowengi duniani wanataka umoja wa Kiislamu na wako katika harakati hiyo ya Umoja inayoongozwa na Iran.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Ayatullah Muhsin Araki ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran katika mkutano na waandishi habari ambapo ametoa maelezo kuhusu mkutano ujao wa Umoja wa Kiislamu.
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu
Ameongeza kuwa, Mkutano wa 33 wa Kimatiafa wa Umoja wa Kiislamu utafanyika Tehran wiki hii huku fikra za ukufurishaji zikiwa zimeshindwa katika jamii za Waislamu duniani na jambo hilo linaashiria mafnaikio makubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wote walio katika harakati ya umoja miongoni mwa Waislamu.
Ayatullah Araki amesema hivi sasa fikra ya umoja zinaenea katika ulimwengu wa Kiislamu na wengi wanaunga mkono fikra hiyo.
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu imeandaa Mkutano wa 33 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ambao umepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran, kuanzia Novemba 14-16 na kuwashirikisha wanazuoni na wasomi wa Kiislamu kutoka nchi 90. Kongamano hilo hufanyika kila mwaka katika Wiki ya Umoja wa Waislamu.
Kuhusu chimbuko la Wiki ya Umoja wa Kiislamu inafaa kuashiria hapa kuwa, Ahlu Suna wal Jamaa wanategemea baadhi ya riwaya katika kuamini kwamba Mtume Mtukufu SAW alizaliwa tarehe 12 Rabiul Awwal nao Waislamu wa madhehebu ya Shia wana riwaya nyingine nyingi zinazowafanya waamini kuwa Mtume SAW alizaliwa tarehe 17 Rabiul Awwal. Kipindi cha kati ya tarehe hizo mbili kilitangazwa na Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu ili kuleta umoja na mfungamano kati ya Waislamu bila kujali madhehebu zao.

3469844

captcha