IQNA

Mgombea urais Algeria: Wote waliohifadhi Qur'ani kikamilifu kupata digrii

12:20 - December 07, 2019
Habari ID: 3472260
Mgombea urais nchini Algeria amesema wote waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu nchini humo watatunukiwa Shahada (digrii) ya Kwanza.

Abdelkader Bengrina amesema iwapo atachaguliwa, atahakikisha kuwa Waalgeria wote waliojifunza na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu watahesabiwa kuwa walio na Shahada ya Kwanza na hivyo  wanaweza kuingia chuo kikuu na kuanza moja kwa moja Shahada ya Uzamili (Masters).

Bengrina anawania urais kwa tiketi ya Chama cha Elbina. Uchaguzi wa rais nchini Algeria umepangwa kufanija Disemba 12,2019.

Algeria ni nchi ya Kiislamu iliyo katika eneo la kaskazini mwa Afrika na asilimi 99 ya wakazi wake ni Waislamu.

3862161

captcha