IQNA

Mkutano wa UAE wajadili nafasi ya dini katika kustahamiliana

18:54 - December 10, 2019
Habari ID: 3472267
TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa sita wa kila mwaka wa Jukwaa la Kustawisha Amani Katika Jamii za Waislamu umefanyika katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mkutano huo wa siku tatu ambao ulianza Jumatatu umewaleta pamoja washiriki 1,000 wakiwemo wanazuoni wa kidni, wasomi na wanafikra kutoka nchi mbali mbali. Mada kuu ya kongamano la mwaka huu ambali limefanika mjini Abu Dhabi ni 'Nafasi ya Dini katika Kueneza Kustahamiliana'.

Akihutubu katika ufunguzi wa kikao hicho Waziri wa Masuala ya Kustahamiliana nchini UAE Sheikh Nahyan bin Mubarak Al Nahyan alisisitiza umuhimu wa kuhurumiana watu kutoka tamaduni na dini mbali mbali.  Amesema UAE inaamini kuwa kustahamiliana ni kati ya mafunzo ya dini tukufu ya Kiislamu.

3863031

captcha