IQNA

Hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky yazidi kuwa mbaya akiwa gerezani

18:16 - January 11, 2020
Habari ID: 3472363
TEHRAN (IQNA) - Ofisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetangaza kuwa, hali ya kiafya ya kiongozi huyo anayeshikiliwa gerezani imezidi kuwa mbaya.

Taarifa ya harakati hiyo iliyoandikwa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter imeeleza kwamba, hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky ni mbaya sana.
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imesema kuwa, taarifa ilizonazo kutoka kwa watu wa karibu waliofanikiwa kukutana na Sheikh Zakzaky zinaonyesha kwamba, hali ya kiafya ya mwanazuoni huyo imezidi kuwa mbaya kuliko hapo kabla.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu (Islamic Human Rights Commission (IHRC)) yenye makao yake London nchini Uingereza, Massoud Shajareh amezungumzia hali mbaya ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe na kusema: "Uwezekano wa kuachiwa huru mwanazuoni huyo ni mdogo sana hasa kwa kutilia maanani mashinikizo makubwa yanayofanywa na utawala wa Nigeria dhidi ya Sheikh Zakzaky."
Sheikh Ibrahim Zakzaky, (66) na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussaynia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi katika shambulio hilo.
Wanaharakati na wapigania haki katika maeneo mbalimbali ya dunia wameendelea kuitaka serikali ya Rais Muhamadu Buhari imuachilie huru Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Itakumbukwa kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky, 66, na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati askari wa jeshi la Nigeria walipovamia na kushambulia Hussainiyah iliyoko katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria wasiopungua 1,000, wakiwemo wana watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi. Sheikh Zakzaky na mke wake walipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na askari wa Nigeria katika tukio hilo.
Baada ya jitihada kubwa, maandamano ya kila pembe na mashinikizo mengi ya ndani na kimataifa, mnamo mwezi Agosti, mahakama ya Nigeria iliruhusu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wapelekwe India kutibiwa, lakini kutokana na matatizo na vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa usalama walioandamana naye, kiongozi huyo wa kidini pamoja na mkewe waliamua kurudi Nigeria baada ya kukaa India kwa muda wa siku mbili tu pasi na kupatiwa matibabu.

3870594

 

captcha