IQNA

Waislamu wa Nigeria walamikia kuendelea kushikiliwa Sheikh Zakzaky

20:37 - January 15, 2020
Habari ID: 3472374
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetoa taarifa kulalimikia hatua ya utawala wa nchi hiyo kuendelea kumshikilia korokoroni kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kufuatia matamshi ya  Gavana wa Jimbo la Kaduna la kaskazini mwa Nigeria  Nasir Ahmad El-Rufai na mwanasheria mkuu wa jimbo hilo Aisha Dikko (Sheikh Zakzaky anashikiliwa katika gereza kuu ya jimbo la Kaduna) wamesema kuwa hatima ya Sheikh Zakzaky na mke wake iko mikononi mwa mahakama na si watawala wa jimbo. Kufuatia kauli ya maafisa hao wawili wa ngazi za juu jimboni Kaduna, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetoa taarifa na kusema: "Wakuu wa jimbo la Kaduna na serikali ya Nigeria wanabeba dhima ya kuendelea kushikiliwa kinyume cha sheria kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na hawapasi kuitwika mahakama jukumu hilo kwa sababu mnamo Disemba 2 2016 Mahakama Kuu ya Nigeria ilitoa hukumu na kusema kukakamtwa na kuwekwa kizuizini Sheikh Zakzaki ni kinyume cha katiba ya Nigeria."

Taarifa hiyo imesema Sheikh Zakzaky ni muathirika wa jinai na hajatenda makossa yoyote na hivyo anakabiliwa na tuhuma zisizo na msingi.

Aidha taarifa hiyo imetoa wito kwa mashirika ya kimataifa na kutetea haki za binadamu kuendeleza mashinikizo dhidi ya serikali ya Nigeria ili imuachilie huru Sheikh Zakzaky anayeshikiliwa kinyume cha sheria.

3871956/

 

captcha