IQNA

Mwanaharakati wa Nigeria

Kuuawa shahidi Lt.Jen. Soleimani kuliwaunganihsa wapigania uhuru duniani

17:45 - January 21, 2020
Habari ID: 3472391
TEHRAN (IQNA) – Mwanaharakati wa Nigeria ambaye ni mwanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) amesema kuuawa shahidi kamanda wa ngazi za juu wa Iran Luteni Jenerali Soleimani kuliwaunganisha wapigania uhuru kote duniani.

Akihutubu katika kongamano 'Haki za Binadamu za Kimarekani kwa Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu' mjini Tehran siku ya Jumanne, Bi. Jumay Ahmed Karoufi alisema Shahidi Soleimani alikuwa na nafasi kubwa katika kuwaunganisha Waislamu duniani.

Huku akilaani vikali mauaji ya Luteni Jenerali Soleimani, mwanaharakati huyo wa Nigeria amesema ugaidi wa Marekani unawalenga Waislamu wote duniani.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine wanane, walishambuliwa tokea angani na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote wakauawa shahidi katika tukio hilo.

Kufuatia ugaidi huo wa Marekani usiku wa kuamkia Jumatano 8 Januari, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC lilizipiga kwa makumi ya makombora, kambi mbili za Marekani nchini Iraq ikiwa ni kujibu jinai ya kigaidi iliyofanywa na askari vamizi wa Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

Kwingineko katika hotuba yake, Bi. Karoufi aliashiria hali ya kiongozi wa IMN Sheikh Ibrahim Zakzaky ambapo amesema sheikhe huyo na mke wake wanahitaji msaada wa dharura wa kiafya.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, (66) na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussaynia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi katika shambulio hilo.
Wanaharakati na wapigania haki katika maeneo mbalimbali ya dunia wameendelea kuitaka serikali ya Rais Muhamadu Buhari imuachilie huru Sheikh Ibrahim Zakzaky.

3873217/

captcha