IQNA

Maandamano makubwa ya kupinga Marekani na kuunga mkono Iran yafanyika Afrika Kusini

18:11 - January 23, 2020
Habari ID: 3472400
TEHRAN (IQNA) – Watu wa matabaka mbali mbali nchini Afrika Kusini wamekusanyika mbele ya Ubalozi wa Marekani mjini Pretoria kulaani sera za Rais Trump wa Marekani dhidi ya Iran.

Maandamano hayo ambayo yameandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini yameitishwa kama njia ya kuoneysha mfungamano na watu wa Iran baada ya Mareknai kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Waandamanaji hao wameonekana wakiwa wamebeba bendera za Iran, Palestina, Hizbullah na pia picha za  Imam Khomeini (MA) na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Pia walikuwa wamebeba picha za Shahidi Qassem Soleimani zilizokuwa zimeandikwa 'Sisi Sote ni Soleimani'.

na Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini, ambacho ni muitifaki wa chama tawala ANC,  kimetoa taarifa na kuitaka serikali ya Trump kuondoa vikwazo dhidi ya Iran, kuacha kueneza vita duniani, kuacha mauaji ya kigaidi, kuheshimu mamlaka ya kujitawala nchi na kuheshimu haki za binadamu na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

برگزاری تظاهرات ضد آمريكايی در پرتوريا

برگزاری تظاهرات ضد آمريكايی در پرتوريا

برگزاری تظاهرات ضد آمريكايی در پرتوريا

برگزاری تظاهرات ضد آمريكايی در پرتوريا

3873740

captcha