IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika Moscow

13:23 - January 27, 2020
Habari ID: 3472409
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yamefanyika katika mji mkuu wa Russia, Moscow katika tawi la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW).

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo ya Qur'ani yamefanyika katika Kituo cha Darul Qur'an cha chuo hicho mjini Moscow kwa lengo la kuwachagua wawakilishi wa Russia katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran.

Washiriki walishindana katika kuhifadhi Qur;ani Tukufu kikamilifu na walioshinda walitunukiwa zawadi.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) kilianzishwa nchini Iran kwa lengo la kueneza mafundisho ya Kiislamu kote dunaini kwa kutumia mbinu za kisasa. Chuo hicho sasa kina matawi maeneo kadhaa duniani.

Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamepengwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad nchini Iran baadaye mwaka huu.

3874172

captcha