IQNA

Makosa zaidi ya 300 katika tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kiebrania iliyochapishwa Saudia

21:00 - January 27, 2020
Habari ID: 3472411
TEHRAN (IQNA) – Tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiebrania iliyochapishwa Saudia Arabia imepatikana ikiwa na makosa zaidi ya 300.

Mtafiti Mpalestina Alaeddin Ahmed, amenukuliwa na tovuti ya Al Jazeera akisema aghalabu ya makosa yanaonekana ni ya makusudi kwani yanaenda sambamba na itikadi za Mayahudi na hivyo ameitathmini hatua hiyo kuwa yenye lengo la kuuridhisha utawala haramu wa Israel. Amesema tarjumi hiyo ina makosa 300 ya wazi ambayo ni kinyume cha itikadi za Kiislamu. Amesisitiza kuwa kuwa makosa hayo yanaonekena kuwa ni mkakati wa makusudi wa kuipotosha Qur'ani Tukufu.

Msomi huyo Mpalestina  ameongeza kuwa: "Tarjumi hii ya Qur'ani ambayo imechapishwa katika Kituo cha Kuchapisha Qur'ani cha Mfalme Fahd mjini Madina imetarjumiwa kwa Kiibrania na mkaazi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) anayejulikana kwa jina Assad Nimer Busool."

Kati ya makosa katika tarjumi hiyo ni upotoshaji wa Aya ya 7 ya Surah Israa ambapo badala ya Msikiti wa Al Aqsa, tarjumi ya Kiibrania imeandikwa Hekalu.

Aidha mtarjumi katika kuendeleza upotoshaji wake hajatumia majina ya Mtume Muhammad SAW na Nabii Isa AS katika tarjumi yake hiyo. Halikadhalika ametaja jina la Ishaq AS pekee kama mwana wa Nabii Ibrahim AS bila kumtaja Ismail AS jambo ambalo linaenda sambamba na itikadi za Kiyahudi.

Mhadhiri Dkt.Mahmoud Refaat naye amesema kuwa ameichunguza tarjumi hiyo kwa makini kwa zaidi ya mwezi moja na amegundua kuwa ina makosa zaidi ya 300.

Tarjumi hiyo ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya  Kiebrania iliyochapishwa katika taasisi rasmi nchini Saudia imeibua gumzo katika mitandao ya kijamii huku kitendo hicho cha upotoshaji wa Qur'ani Tukufu kikilaaniwa vikali na miito ikitolewa ya kuchukuliwa hatua za dharura kurekebisha makosa hayo.Makosa zaidi ya 300 katika tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya  Kiebrania iliyochapishwa Saudia

3874483

captcha