IQNA

Hamas yatoa wito kwa Wapalestina kusimama kidete dhidi ‘Mumala wa Karne’

13:02 - February 10, 2020
Habari ID: 3472458
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, mipango ya Marekani na utawala ghasibu wa Israel na ushirikiano wao mkubwa wa kutekeleza mpango wa Muamala wa Karne na kuchora ramani mpya ya kuliunganisha eneo la Ukingo wa Magharibi na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, utafeli na kushindwa.

Fauzi Barhum amesema Palestina itaendelewa kuwa mali ya taifa la Palestina na kuongeza kuwa, Wapalestina wameungana na wamesimama kidete kwa ajili ya kukabiliana na mpango wa Muamala wa Karne.

Wakati huo huo harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina za Hamas na Fa'th zimefikia makubaliano ya kuimarisha umoja na mshikamano kwa ajili ya kukabiliana na mpango wa Kimarekani-Kizayuni wa Muamala wa Karne.

Itakumbukwa kuwa tarehe 28 mwezi uliopita wa Januari Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu walizindua mpango eti wa amani wa Muamala wa Karne.

Tarehe 28 Januari, rais Donald Trump wa Marekani akiwa pamoja na waziri mkuu wa utawala bandia wa Israel, Benjamin Netanyahu alizindua mpango wa ubaguzi wa kimbari wa Muamala wa Karne.

Kuitambua rasmi Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni, kuupatia utawala huo haramu umiliki wa asilimi 30 ya eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, kupingwa haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea nchini kwao na kupokonywa silaha kikamilifu ile itakayoitwa nchi ya Palestina ni miongoni mwa vipengele vya mpango huo wa udhalilishaji.

3470593

captcha